26 Juni 2025 - 18:28
Taarifa ya Kikosi cha Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na Uadui wa Israel: "Hadhi ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu imeongezeka"

"Mashambulizi ya Iran kwa Utawala haram wa Kizayuni (Israel) yameongeza Hadhi ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu na Kufuta Hadithi feki za Siku zote kwamba: Israel ina Jeshi lisiloshindwa".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kikosi cha Kijeshi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (Guard Revolutionary Corps - IRGC) kimetoa taarifa ya tamati kuhusiana na mashambulizi ya Uadui ya utawala wa Kizayuni.

Taarifa ya Kikosi cha Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na Uadui wa Israel: "Hadhi ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu imeongezeka"

Sehemu ya taarifa hiyo imeeleza kama ifuatavyo:

"Miongoni mwa mafanikio makubwa ya hatua hii ya majibu ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Israel ni:

1_Kuimarisha umoja wa kitaifa.

2_Kuongeza imani ya Wananchi kwa  jeshi lao la kulinda Mapinduzi ya Kiislamu.

3_Kufichua mitandao ya uharibifu, ugaidi na ujasusi ndani ya nchi.

4_Kuinua hadhi ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu.

5_Kufichua uongo wa hadithi feki ya Kizayuni isemayo: “Israel ina Jeshi lisiloshindika”

6_Kuanguka kwa mifumo yote ya ulinzi wa anga ya adui, ambayo ilikuwa na gharama kubwa, lakini haikuweza kuzuia Makombora ya Iran yenye teknolojia ya hali ya juu.

7_Kuweka matumaini katika mioyo ya wanyonge na wadhulumiwa duniani katika kupambana na watawala wa dhulma.
8_Hata kuingilia kati kwa jeshi la Marekani ili kuisaidia Israel iliposhindwa na kuishiwa nguvu mbele ya Mashambulizi ya Iran, hatua hiyo haikuweza kubadilisha mlinganyo wa nguvu za kijeshi, na jibu la Iran kupitia “Operesheni Bisharat al-Fat'hi / Bishara ya Ushindi” liliilenga na kuichakaza kambi ya jeshi la Marekani ya Al-Udeid, huko Qatar, na hatimaye pigo hilo kwa mara nyingine tena likawasilisha ujumbe wa nguvu za kijeshi wa Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha